Alhamisi 11 Juni 2026 - 18:15
Mhimili wa Muqawama Hauko Peke Yake

Hawza/ Kundi la “Marafiki wa Muqawama wa Uturuki” limefanya mkusanyiko wa maandamano mbele ya ubalozi mdogo wa Israel mjini Istanbul na kutangaza uungaji mkono wake kwa Ghaza na Lebanon, washiriki walisisitiza mshikamano wao na mataifa ya eneo hilo dhidi ya Israel kwa kupaza kauli mbiu isemayo: “Mhimili wa Muqawama hauko peke yake.”

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu Islami Analysis, mjini Istanbul, kundi la “Marafiki wa Muqawama wa Uturuki” liliandaa maandamano kuelekea mbele ya ubalozi mdogo wa Israel na kutangaza uungaji mkono wake kwa wananchi wa Ghaza na Lebanon.

Katika mkusanyiko huo, ambao ulihudhuriwa na wanaharakati na wafuasi wa Palestina, washiriki walionesha mshikamano wao na muqawama wa Palestina na Lebanon kwa kupaza kauli mbiu isemayo: “Mhimili wa Muqawama hauko peke yake.”

Katika taarifa iliyosomwa na Akram Ekşi, baba wa shahidi wa tarehe 15 Julai, Kemal Ekşi, kulisisitizwa umuhimu wa kuunga mkono mhimili wa muqawama na ulazima wa kusimama dhidi ya hatua za Israel.

Washiriki wa mkusanyiko huo huku wakirejelea maendeleo ya hivi karibuni katika eneo hilo, walitangaza kwamba: Ghaza, Lebanon na Iran ziko katika safu moja ya pamoja dhidi ya Marekani na Israel.

Wakati wa hafla hiyo pia, bendera za Marekani na Israel ziliwekwa chini ardhini, na waandamanaji walizikanyaga ili kuonesha upinzani wao dhidi ya sera za nchi hizo mbili.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha